1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT:Mapambano yaendelea nchini Lebanon

21 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG5V

Vikosi vya Israel vimefanya mashambulio ndani ya mpaka wa Lebanon,mapambano yakizidi kushika kasi nchini humo.Si chini ya wanajeshi 2 wa Kiisraeli na wapiganaji 2 wa Hezbollah waliuawa katika mapambano hayo.Israel inadai kuwa mashambulio yake ya angani kwa hivi sasa yamepunguza kwa nusu uwezo wa kijeshi wa Hezbollah.Hayo lakini yamekanushwa na kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah aliejitokeza kwenye televisheni ya Kiarabu ya Al Jazeera,siku moja baada ya Israel kusema kuwa imewapiga mabomu wakuu wa Hezbollah.Watu 300 wameuawa nchini Lebanon tangu mashambulio kuanza nchini humo.Kaskazini mwa Israel pia watu 29 wameuawa.