BEIRUT:majeshi ya Israel yaondoka kusini mwa Lebanon
1 Oktoba 2006Matangazo
Majeshi ya Israel yamekamilisha zoezi la kuondoka kusini mwa Lebanon na kukabidhi udhibiti wa sehemu hiyo kwa majeshi ya Lebanon na ya majeshi ya kimataifa ya kulinda amani nchini humo.
Hatua ya Israel kuondoa majeshi hayo ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa kwa mujibu wa azimio la Umoja wa Mataifa juu ya kusimamisha vita nchini Lebanon baina ya Israel na wapiganaji wa Hezbollah.
Israel ilipeleka askari alfu 10 nchini Lebanon kabla ya makubaliano hayo kufikiwa.