BEIRUT,Majeshi ya Israel yamo ndani ya Lebanon
25 Julai 2006Matangazo
Majeshi ya Israel sasa yamo ndani ya Lebanon licha ya kukabiliwa na upinzani mkali wa wapiganaji wa Hezbollah.
Katika mapambano na wapiganaji hao wa Hezbollah Israel ilipoteza askari wake wawili. Majeshi ya Israel pia yamearifu kuwa helikopta yao moja ilianguka kutokana na sababu zisizojulikana.
Marubani wote wawili wa helikopta hiyo pia wamekufa.