1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut:Maafisa wa Ujerumani kuwasili Lebanon kumuhoji mtuhumiwa.

25 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDIE

Wachunguzi wa kipelelezi wa Ujerumani wapo nchini Lebanon kuungana na maafisa wa upelelezi wa huko kumuhoji mtuhumiwa wa aliyeweka bomu katika kituo cha treni lililoshindwa kuripuka mwezi uliopita.

Mtuhumiwa huyo wa pili wa kilebanon katika tukio hilo alijipeleka mwenyewe kwa maafisa wa polisi katika mji wa Tripoli nchini Lebanon hapo jana.

Maafisa nchini Ujerumani vile vile wanataka kijana huyo mwenye miaka 20 arejeshwe nchini Ujerumani kwa ajili ya kushtakiwa.

Kijana mwengine wa kilebanon mwanafunzi mwenye miaka 21 aliyepandikiza bomu lililoshindwa nalo kuripuka alikamatwa jumamosi iliyopita kaskazini mwa Ujerumani katika mji wa Kiel.

Watu hao wawili wanashtumiwa kupandikiza mabomu yaliyoshindwa kuripuka katika vituo vya treni vya kuelekea Dortmund na Koblenz July 31.