1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT.Lebanon yaomboleza kifo cha waziri wake wa viwanda Pierre Gemayel

22 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqL

Lebanon imeanza maombolezo ya siku tatu kufuatia kifo cha aliyekuwa waziri wa viwanda Pierre Gemayel.

Licha ya kutolewa miito ya kudumisha utulivu kifo cha mwanasiasa huyo aliyepinga sera za Syria nchini Lebanon huenda kikazidisha hali ya wasiwasi nchinbi humo.

Hadi sasa mawaziri watano wanopinga hatua ya Syria ya kujiingiza katika maswala ya Lebanon wameuwawa katika kipindi cha m iaka miwili.

Wafuasi wa aliyekuwa waziri wa viwanda Pierre gemayel wanailaumu Damascus kwa mauaji hayo na pia wanahofia kuwa kitendo hicho kinadhamiria kuitoa madarakani serikali ya waziri mkuu Fuad Siniora.

Rais George W Bush wa Marekani pia ana maoni sawa na wafuasi wa Gemayel.

O ton…Na tunawaunga mkono katika juhudi za kulinda demokrasia huku wakikabiliwa na majaribio kutoka Syria na Iran pamoja na washirika wao katika njama za kuvuruga utulivu na kuchochea machafuko katika nchi hiyo mashuhuri. Natoa mwito wa kuanzishwa uchunguzi wa kina utakaowezesha kuwakamata wale waliohusika na mauaji hayo na wakati huo huo naiomba jamii ya kimataifa iiunge mkono serikali ya waziri mkuu Fuad Siniora.