Beirut.Kikosi cha wanajeshi wa majini cha Ujerumani kupelekwa Lebanon.
8 Septemba 2006Waziri wa masuala ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier anatumai kuwa kikosi cha wanamaji wa Ujerumani kitapelekwa Lebanon licha ya matatizo ya hivi sasa.
Alisema, ana hakika kwamba suluhisho litapatikana kuhusu ujumbe huo, lakini kwanza masharti ya yanayohusika na tume hiyo yanapaswa kujadiliwa na Umoja wa Mataifa, ili kuweza kuzuia usafirishaji wa silaha za magendo kwa njia ya maana.
Steinmeier akaongezea kwa kusema.
„ Ni matumaini yangu kuwa utaratibu huo hautachukua muda mrefu san, ili sisi huku Ujerumani tupate kupitisha maamuzi ya kisiasa yanayohitajika“.
Aidha waziri Steinmeier hapo jana alifanya ziara fupi katika mji mkuu wa Beirut nchini Lebanon, ambako amekutana na waziri Mkuu wa nchi hiyo Fuoad Siniora na maafisa wengine wa serikali.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya habari ni kwamba waziri Siniora amuntumia barua katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan kuiomba Ujerumani ishiriki katika jeshi la kulinda amani nchini Lebanon.