1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT:Generali wa Zamani mkristo,Michel Aoun na orodha yake washinda uchaguzi Lebanon

13 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF3o

Generali wa Zamani mkristo Michel Aoun ambaye amerejea kutoka mafichoni wiki kadhaa zilizopita amepata ushindi wa ghafla katika duru ya tatu ya Uchaguzi wa bunge nchini Lebanon.

Matokea rasmi yameonyesha orodha ya Wagombea wanaongozwa na Michel wamepata ushindi katika eneo hilo muhimu nchini Lebanon.

Hata hivyo haijaeleweka ushindi huo unaamaanisha nini kwa juhudi za upinzani za kuchukua madaraka kutoka kwa washirika wa Syria.

Viti 58 kati ya viti 128 vya bunge vilikuwa vinagombaniwa katika uchaguzi huo wa jumapili katika eneo la kati na mashariki mwa Lebanon.