1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT:Chama cha Upinzani chadai ushindi nchini Lebanon

20 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF1f

Chama kikuu cha upinzani nchini Lebanon kinachoipinga Syria,kimedai ushindi wa uchaguzi wa hapo jana.

Saad Al Hariri mwananwe waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Rafiq Harii ameahidi kuleta mageuzi baada ya matokeo ambayo siyo rasmi kuonyesha muungano wake umeshinda viti vyote 28 vilivyokuwa vimebakia katika eneo la kaskazini.

Uchaguzi huo uliofanyika kwa muda wa wiki nne ndio wa kwanza kuwahi kufanyika nchini humo tangu kuondoka kwa wanajeshi wa Syria mnamo mwezi Aprili.

Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa baadae hii leo