1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Wito kusuluhisha mgogoro wa Lebanon

28 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBeO

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa,Bernard Kouchner amewahimiza viongozi wa Lebanon kutenzua tofauti zao kwa kufanya majadiliano mapya.Tangu siku ya Ijumaa,Kouchner anakutana na viongozi wa wa Lebanon wa vyama mbali mbali vya kisiasa.Azma ya majadiliano hayo ni kutafuta njia ya kusuluhisha mgogoro wa kisiasa nchi humo. Tangu miezi minane iliyopita,kinyanganyiro cha mamlaka kinaendelea kati ya serikali ya wengi walio dhidi ya Syria na upande wa upinzani unaoiunga mkono Syria.Suala mojawapo kuu katika mgogoro wa pande hizo mbili ni linahusika na kuruhusu Mahakama ya Kimataifa kuchunguza mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon,Rafik Hariri.Wafuasi wa marehemu Hariri wanaishuku Syria kuhusika na mauaji hayo.