BEIRUT : Waziri wa viwanda auwawa
21 Novemba 2006Matangazo
Waziri wa viwanda nchini Lebanon Pierre Gemayel ameuwawa na watu wenye silaha karibu na Beirut leo hii.
Duru za usalama zimesema watu hao wenye silaha waliushambulia kwa risasi msafara wake wakati ukipita kwenye kitongoji cha Wakristo cha Sin el Fil.
Gemayel alikimbizwa hospitali ambapo baadae alikufa kutokana na majeraha ya risasi.