1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT : Waziri wa ulinzi wa Ujerumani yuko Lebanon

3 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwY

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Joseph Jung amewasili katika mji mkuu wa Lebanon Beirut kwa mazungumzo na maafisa wa serikali ya Lebanon kuhusiana na shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa zinazoongozwa na kikosi cha wanamaji cha Ujerumani kupiga doria katika mwambao wa Lebanon.

Baadae ataondoka kuelekea Tel Aviv kwa mazungumzo na waziri mwenzake wa ulinzi Amir Peretz.Mazungumzo hayo yatalenga tukio la wiki iliopita ambapo kwayo ndege za Israel zilitishia manowari ya Ujerumani.

Msemaji wa jeshi la Israel baadae alisema hatua hiyo ilitokana na helikopta ya Ujerumani kuruka kutoka kwenye manowari hiyo karibu na mpaka wa Israel na Lebanon bila ya kuitaarifu Israel na mapema.