BEIRUT :Waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora aitolea mwito tena jumuiya ya kimataifa
20 Julai 2006Waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora kwa mara nyingine tena ameitolea mwito jumuiya ya kimataifa kuingilia kati na kumaliza mashambulio yanayofanywa na Israel dhidi ya nchi yake Lebanon.
Akizungumzia juu ya hali ilivyo ikiwa mgogoro huo leo umeingia siku yake ya tisa anasema.
’’Kila mmoja anafahamu juu ya mashambulio ya Israel dhidi ya Lebanon ambayo yamesababisha hasara kubwa.Idadi ya watu waliokuwa imefikia kiwango cha kutisha.’’
Hadi kufikia sasa waziri mkuu huyo wa Lebanon amesema zaidi ya watu 300 wameuwawa na wengine 1000 wamejeruhiwa nchini humo.
Lakini naibu waziri mkuu wa Israel Shimon Peres ameitilia shaka idadi hiyo iliyotolewa na Lebanon akisema kuwa haiwezi kuaminika kabisa.
Nchini Israel watu 29 wameuwawa.Wakati huo huo mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Javier Solana yupo Israel na atafika maeneo mengine ya Palestina kwa ajili ya mazungumzo ya kuutatua mgogo wa sasa mashariki ya kati na waziri mkuu Ehud Olmert wa Israel na rais wa Palestina Mahmoud Abbas.