BEIRUT : Waziri Mkuu wa Lebanon aunda serikali
19 Aprili 2005Matangazo
Waziri Mkuu mteule wa Lebanon Najib Mikati ameunda serikali mpya ambayo anasema imeyaunganisha makundi yote.
Msemaji wake amesema serikali hiyo itajumuisha mawaziri 14 kutoka ulimwengu wa kisiasa na biashara.Baraza hili jipya la mawaziri litatangazwa rasmi baadae leo hii.Hatua hiyo inaweka uwezekano mkubwa wa kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mwezi ujao kama ilivyopangwa.
Lebanon imekuwa haina serikali tokea mwezi wa Februari wakati nchi hiyo ilipotumbukia kwenye machafuko ya kisiasa kufuatia kuuwawa kwa waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Rafik al Hariri.