1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT. Waziri mkuu wa Lebanon ajiuzulu tena.

14 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFNV

Waziri mkuu wa Lebanon anaeungwa mkono na Syria Omar Karami amejiuzulu kwa mara ya pili katika wiki sita baada ya kushindwa kuunda serikali.

Omar al Karami amesema kuwa kujiuzulu kwake hakutakuwa pingamizi la uchaguzi mkuu unaotazamiwa kufanyika mwezi may, ingawa wadadisi wanasema kuwa kujiuzulu kwake kumezidi kuitumbukiza Lebanon katika dimbwi la kisiasa hasa kufuatia kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri.

Vilevile huenda uchaguzi huo ukachelewa kwa mawiki au hata miezi kutokana na kuwa Lebanon bado haijafaulu kuunda baraza la mawaziri hadi kufikia sasa.

Rais Emile Lahoud atafanya mazungumzo na wanasheria hapo kesho ili kumchagua waziri mkuu mwingine.