1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Watuhumiwa wa tuhuma za ulipuaji wa mabomu nchini Ujerumani kushtakiwa Lebanon.

3 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDFi

Maafisa nchini Lebanon wamewafikisha mahakamani watuhumiwa watano wa jaribio la mauaji na kuchoma moto wakihusika na mpango wa shambulio la bomu katika vituo vya treni nchini Ujerumani mwezi Julai.

Watatu kati yao, wote raia wa Lebanon , walikamatwa nchini humo wakati mmoja ambaye pia ni Mlebanon na raia mmoja wa Syria wanashikiliwa nchini Ujerumani.

Mwendesha mashtaka mkuu wa Lebanon amekataa kuwapeleka watuhumiwa hao nchini Ujerumani, akisema kuwa watakabiliwa na mashtaka na kuhukumiwa nchini Lebanon.

Katika mahojiano na gazeti la Ujerumani la Focus, polisi wa Ujerumani wamesema kuwa watuhumiwa hao wa mpango wa shambulio la bomu walikuwa wanahamasika kufanya kitendo hicho kutokana na hasira juu ya kuchapishwa kwa katuni za kumdhihaki Mtume Mohammed katika vyombo vya habari vya Ujerumani.

Mabomu hayo yaliyofichwa katika treni mbili nchini Ujerumani yalishindwa kulipuka kwasababu ya mapungufu katika vifaa vyake vya kulipua.