BEIRUT: Wasi wasi wa kuzuka machafuko Lebanon
19 Machi 2005Matangazo
Waziri mkuu Emile Lahoud wa Lebanon ametoa wito kwa wanasiasa wa upinzani na wale wanaoiunga mkono Syria wakutane moja kwa moja.Wito huo umetolewa baada ya bomu kuripuka mjini Beirut katika eneo ambako huishi wakaazi wengi wa kikristo.Hakuna alieuawa katika shambulio hilo lakini watu sita walijeruhiwa.Syria ikiendelea kuviondosha vikosi vyake kutoka Lebanon baada ya kuwepo nchini humo kwa takriban miaka 30,kuna wasi wasi kwamba ghasia zaidi huenda zikazuka kwa sababu ya mivutano ya kisiasa inayoongezeka.