BEIRUT: Wanamgambo wapambana na vikosi vya Lebanon
3 Juni 2007Matangazo
Vikosi vya serikali nchini Lebanon vinaendelea kupambana na wanamgambo wa kundi la Fatah al-Islam waliojificha katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Nahr al-Bared,kaskazini mwa nchi. Duru za usalama zinasema,wanamgambo wa Fatah al-Islam wanaendelea kukabiliana na mashambulizi ya majeshi,lakini mashahidi wengine wanasema, mapigano ya mapema leo hii hayakuwa makali kulinganishwa na siku mbili zilizopita.Tangu vikosi vya serikali kuanza kushambulia upya siku ya Ijumaa,sehemu nyingi za kambi hiyo zimeteketezwa.Baadhi kubwa ya wakazi 40,000 wa kambi hiyo wamekimbilia kwengine.