1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut. Wanajeshi wa mwisho wa Syria waondoka nchini Lebanon.

26 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFJ6

Wanajeshi 200 wa mwisho wa Syria waliokuwa nchini Lebanon wameondoka nchini humo, na kumaliza kuwako kwa majeshi ya nchi hiyo ambako kulidumu kwa zaidi ya miaka 30.

Hii imefuatia sherehe iliyofanyika katika kituo cha anga cha kijeshi cha Riyyak katika eneo la mashariki ya bonde la Bekaajkuadhimisha kukamilika kwa kuondolewa kwa majeshi ya Syria kutoka Lebanon.

Hii inaiweka Syria katika njia sahihi ya kukubaliana na azimio la umoja wa mataifa linalotaka majeshi yote yaliyoko nchini Lebanon kuondolewa.

Majeshi ya Syria yalitumwa kwa mara ya kwanza katika nchi hiyo wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Lebanon katika mwaka 1976.

Shinikizo la kimataifa dhidi ya Syria kuondoa majeshi yake lilizidi baada ya kuuwawa kwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri miezi miwili iliyopita. Wengine wamekuwa wakiishutumu Syria kwa mauaji hayo.