Beirut. Wanajeshi wa mwisho wa Syria waondoka Lebanon
26 Aprili 2005Matangazo
.
Wanajeshi wa Syria wameondoka katika makao yao makuu nchini Lebanon katika mji wa mpakani wa Anjar, na kukamilisha kuondoka kwa majeshi ya Syria kutoka Lebanon. Wakati udhibiti wa Syria wa miaka 29 katika taifa la Lebanon ukimalizika jana, mkuu wa usalama aliyewekwa na mataifa hayo ya Syria na Lebanon , Jamil Sayyed amejiuzulu. Kiongozi wa masuala ya usalama wa Syria nchini Lebanon Rustum Ghazaleh, anatarajiwa purejea leo kwa ajili ya sherehe ya kuwaaga kiasi cha wanajeshi 200 ambao wamebaki nchini Lebanon.