1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut: Wanajeshi wa Lebanon wawapiga risasi waandamanaji wa Kipalestina.

30 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnA

Wanajeshi wa Lebanon wamewaua kwa kuwapiga risasi waandamanaji wawili wa Kipalestina na wakawajeruhi wengine ishirini viungani mwa kambi ya wakimbizi ya Badawi kaskazini mwa nchi hiyo.

Msemaji wa kijeshi amesema wanajeshi hao walipiga risasi hewani kuwazuia waandamanaji kuharibu kizuizi cha kijeshi.

Wapalestina hao walikuwa wakiandamana wakitaka vita vikomeshwe kati ya wanajeshi wa nchi hiyo na wanamgambo wa Fatah al-Islam katika kambi ya karibu ya Nahr al-Barid.

Kufikia sasa watu zaidi ya mia moja na sitini wanakadiriwa wameuawa kwenye mapigano yanayoendelea katika kambi hiyo ya Nahr al-Barid.