BEIRUT: Wanajeshi na wanamgambo wapambana Lebanon
3 Juni 2007Matangazo
Nchini Lebanon,vikosi vya serikali vimepambana vikali na wanamgambo wa kundi la Fatah al-Islam waliojificha katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina Nahr al-Bared.Kwa mujibu wa ripoti za waandishi wa habari,milio ya risasi ilisikika ikitokea kambini na vikosi vya serikali vilirusha makombora.Wakati wa usiku,vikosi hivyo vilitumia vifaru na helikopta ili kuwashinikiza zaidi wanamgambo waliojificha katika kambi hiyo.Tangu siku ya Ijumaa peke yake,zaidi ya watu 20 wameuawa katika mapigano hayo kaskazini mwa Lebanon.Wanajeshi 6 ni miongoni mwa wale waliouawa.