BEIRUT : Waandamanaji wakutane kujadili mgogoro wa Lebanon
11 Desemba 2006Matangazo
Maandamano yakiendelea nchini Lebanon dhidi ya serikali,waziri mkuu Fouad Siniora ametoa mwito kwa wapinzani wake kukutana kutafuta suluhisho la kisiasa.Amesema,waandamanaji waache kuandamana na watumie njia za kisheria kwa kukutana na kuujadili mgogoro wao.Tangu mwanzo wa mwezi wa Desemba,waandamanaji wanaoiunga mkono Syria wamekusanyika kati-kati ya mji mkuu Beirut, kumshinikiza Siniora aondoke madarakani.Baada ya mawaziri sita wa Kishia wa chama cha Hezbollah kujiuzulu,serikali ya Fouad inayoungwa mkono na nchi za magharibi,sasa ina viongozi walio dhidi ya Syria tu.