1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Viti vya wanasiasa waliouawa vyagombewa Lebanon

5 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbs

Wapiga kura nchini Lebanon hii leo wanawachagua wajumbe watakaochukua nafasi za wanasiasa wawili waliouawa.Kiti kimoja kilichokuwa kimeshikwa na aliekuwa waziri wa viwanda,Pierre Gemayel ni mtihani muhimu kwa jumuiya ya Wakristo ya Lebanon iliyogawika.Chaguzi hizo zinafanywa chini ya ulinzi mkali,huku vitisho na mapigano yakiendelea kati ya makundi mbali mbali.

Serikali ya Waziri Mkuu Fouad Siniora,inayoungwa mkono na nchi za Magharibi imeitisha chaguzi hizo bila ya idhini ya rais inayohitajiwa.Viti vinavyogombewa vilikuwa vya wanachama wa muungano unaoipinga Syria na walikuwa wahanga wa kinyanganyiro cha madaraka kinachoendelea kuigawanya Lebanon.