BEIRUT. Viongozi wa upinzani wakutana nchini Lebanon.
3 Machi 2005Matangazo
Viongozi wa upinzani nchini Lebanon wametoa mwito wa kuondoshwa kwa wamajeshi alfu 14 wa Syria waliomo nchini humo.
Baada ya mkutano wao viongozi wapatao sabini wa upinzani wamesema katika tamko lao kwamba pia wanataka Syaria iondoshe idara zake zote za upelelezi na wakuu wa usalama wanaoungwa mkono na Syria wajiuzulu.
Wapinzani hao pia wamesema kwamba ili mazungumzo juu ya kuunda serikali mpya nchini Lebano yafanyike rais Emile Lahoud anapaswa kukubali masharti hayo.