1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT : Usitishaji wa mapigano waanza kufanya kazi

15 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDLN

Maelfu ya wakimbizi waelekea nyumbani kusini mwa Lebanon leo hii wakati usitishaji wa mapiganom kati ya Israel na Hizbollah ukiingia katika siku yake ya pili na vikosi vya Israel vikianza kujitowa katika baadhi ya maeneo iliyokuwa imeyakalia kwa mabavu.

Jana usiku majeshi ya Israel yameondoka kwenye mji wa kusini wa Wakristo wa Marjayoun ambao waliutwaa hapo Alhamisi. Mashahidi baadae wamesema pia wanajeshi hao wamekuwa wakiondoka katika mji wa Qlaiah.

Maafisa wa Israel na wanadiplomasia wa nchi za magharibi wanasema Jeshi la Israel ambalo liliteremsha wanajeshi 30,000 kusini mwa Lebanon kupambana na Hizbollah linapanga kukabidhi baadhi ya maeneo iliyoyateka kwa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa katika siku mbili tatu zijazo.

Marais wa Iran na Marekani wamelaumiana kwa kuchochea mzozo huo.

Wakati huo huo mmojawapo wa masheikh waandamizi wa msimamo mkali nchini Iran ameonya leo hii kwamba iwapo Iran itashambuliwa na Marekani na Israel italipiza kwa mashambulizi ya makombora ya masafa marefu dhidi ya Tel Aviv

Ayatollah Ahmad Khatami mjumbe wa Baraza la Wataalamu nchini Iran amesema iwapo Marekani na Israel zinataka kufanya uchokozi dhidi ya Iran zinapaswa kuogopa siku ambayo makombora yao yanayoweza kurushwa kwa umbali wa kilomita 2,000 kupiga kitovu cha Tel Aviv.