BEIRUT: Uchaguzi wa mwanzo kuchagua bunge la Lebanon
29 Mei 2005Matangazo
Nchini Lebanon,hii leo kunapigwa kura katika duru ya mwanzo ya uchaguzi wa bunge.Kwanza uchaguzi huo unafanywa katika mji mkuu Beirut.Maeneo mengine yatapiga kura jumapili zingine zinazofuata,katika chaguzi zinazofanywa kwa awamu nne.Inadhaniwa kuwa katika mji wa Beirut,orodha ya Saad Hariri,mwana wa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon alieuawa,Rafik Hariri,itapata ushindi.