Beirut. Uchaguzi unaendelea nchini Lebanon ikiwa ni duru ya mwisho ya kulichagua bunge.
19 Juni 2005Uchaguzi unaendelea kaskazini ya Lebanon kwa ajili ya duru ya mwisho ya uchaguzi wa wabunge.
Ni uchaguzi wa kwanza tangu Syria kuondoa majeshi yake kutoka Lebanon baada ya miongo mitatu.
Kiasi cha watu 700,000 katika maeneo mawili ya kaskazini mwa Lebanon wanahaki ya kuwachagua Waislamu 13 na Wakristo 15 watakaokuwa wabunge katika bunge lenye viti 128.
Orodha ya Saad Hariri , ambaye kifo cha baba yake Rafik hariri mwezi wa Februari kilizusha kampeni dhidi ya Syria, inahitaji kiasi cha viti 21 kati ya viti 28 ili kujihakikishia udhibiti wa bunge.
Upigaji wa kura ulianzia mjini Beirut hapo May 29, na kuendelea upande wa kusini, katika eneo la Metn pamoja na uwanda wa kusini wa bonde la Bekaa.