BEIRUT: Uchaguzi nchini Lebanon baada ya kumalizika enzi ya Syria
29 Mei 2005Matangazo
Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa mji mkuu wa Lebanon,Beirut kwa duru ya kwanza ya uchaguzi mkuu nchini humo.Kwa mara ya mwanzo tangu miongo mitatu,uchaguzi safari hii unafanywa bila ya Syria kuwepo nchini humo.Upande wa upinzani unaoipinga Damascus unatazamiwa kushinda.Uchaguzi unafanywa kwa awamu nne katika kipindi cha majuma machache