1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Tarehe ya uchaguzi wa bunge yatangazwa,Lebanon

28 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFIg

Waziri wa mambo ya ndani wa Lebanon Hassan Sabeh ametangaza uchaguzi wa bunge utafanyika kati ya tarehe 29 mwezi Mei na Juni 19.

Kabla ya hapo serikali ya waziri mkuu Nagib Nikat ilishinda kwa idadi kubwa ya kura ya kuwa na imani nayo bungeni.

Kura 109 ziliiunga mkono serikali mpya dhidi ya kura moja tu iliyopinga na tatu hazikupigwa.

Bwana Nikati alianza kuunda serikali mpya wiki iliyopita baada ya miezi miwili ya wimbi la kisiasa.