BEIRUT : Syria yatakiwa kuondoka Lebanon
22 Februari 2005Matangazo
Maelfu ya waandamanaji wameandamana mjini Beirut hapo jana kuongeza shinikizo kwa Syria kuondowa wanajeshi wake walioko nchini Lebanon.
Maandamano hayo yanakuja wiki moja baada ya kuuwawa kwa Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri ambapo watu wengi wanaamini aliuwawa kwa agizo la Syria. Syria imekanusha kuhusika katika mripuko wa bomu uliomuuwa Hariri.
Waandamanaji hao pia wametaka kujiuzulu kwa serikali ya Lebanon inayoungwa mkono na Syria pamoja na kuondolewa kwa wanajeshi wa Syria wanaokadiriwa kufikia 14,000 kutoka ardhi ya Lebanon.