1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Syria yashinikizwa kuondoka Lebanon

3 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFa2

Viongozi wa upinzani nchini Lebanon wanaendelea kuishinikiza Syria kuondosha vikosi vyake vyote pamoja na idara zake zote zinazoendesha shughuli za kiusalama nchini humo.

Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano wa viongozi takriban ya 70 wa upinzani uliofanyika nje ya mji wa Beirut,iliandamana pamoja na orodha ya masharti ambayo ni pamoja na kumtaka mkuu wa usalama anayeungwa mkono na Syria ajiuzulu.

Taarifa hiyo pia imetaka rais Emile lahoud ambaye ni mshirika wa Syria kukubaliana na masharti ya upinzani kabla ya kujiunga na mazungumzo juu ya kuunda serikali mpya ya Lebanon.

Viongozi wa Marekani pamoja na wa mataifa ya Ulaya pia wameitaka Syria kuondosha vikosi vyake nchini Lebanon.Rais Gorge Bush ameishutumu Syria kwa kuingilia masuala ya siasa ya Lebanon.