BEIRUT : Syria yaondowa vikosi Lebanon kaskazini
12 Machi 2005Syria imekamilisha kuondowa takriban vikosi vyake yote katika eneo la kaskazini mwa Lebanon kufuatia miongo kadhaa ya kulikalia eneo hilo.
Hata hivyo inasemekana baadhi ya maafisa wake wa ujasusi bado wangalipo katika eneo hilo na wanajeshi wake kadhaa wapo katika maeneo mengine ya Lebanon.Kuondolewa kwa wanajeshi hao ni utekelezaji wa mpango wa kuviondowa vikosi hivyo kwa awamu uliokubaliwa mapema wiki hii kati ya viongozi wa nchi hizo mbili.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Terje Roed Larsen yuko nchini Syria kwa mazungumnzo na Rais Bashar al Assad. Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa anatazamiwa kuishinikiza Syria kutii Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaloitaka Syria kukomesha udhibiti wake wa kijeshi katika nchi hiyo jirani.