1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT. Rais wa Lebanon akutana na wabunge kumchagua waziri mkuu mpya.

15 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFMl

Rais wa Lebanon Emile Lahud anafanya mazungumzo na wabunge yanayolenga kumteua waziri mkuu mpya atakayeliongoza taifa hilo kuelekea uchaguzi wa bunge mwezi ujao. Duru za kisiasa zinasema waziri wa ulinzi anayeegemea upande wa Syria, Abdel Rahim Mrad, na waziri wa zamani Najib Mikatti wana nafasi nzuri ya kuchaguliwa kuchukua wadhifa huo. Upinzani unamuunga mkono Mikatti. Lebanon imekuwa bila serikali tangu mwisho wa mwezi Februari wakati waziri mkuu Omar Karami alipojiuzulu, majuma mawili baada ya kuuwawa kwa waziri mkuu wa zamani Rafik Hariri. Juzi Jumatano Karami alifutilia mbali mpango wake wa kuunda serikali mpya.