1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Raia waendelea kuhamishwa kutoka Lebanon

19 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG61

Huku mapigano yakiendelea kusini mwa Lebanon, Marekani na mataifa mengine yameendelea kuwaondoa raia wao kutoka Lebanon. Zaidi ya wamarekani 2,400 watahamishwa kwa ndege na meli leo kati ya wamarekani wote 8,000 wanaotakiwa kuondolewa nchini Lebanon.

Meli tatu zilizokuwa zimewabeba raia 1,500 wa Uingereza na mataifa mengine ya Ulaya, zimewasili katika kisiwa cha Cyprus mapema leo.

Waziri mkuu wa Uingereza, bwana Tonya Blair, amesema waingereza 5,000 watahamishwa kufikia mwishoni mwa juma hili.

Umoja wa Mataifa umeonya juu ya mkasa mkubwa wa kibinadamu ambao tayari umewalazimu watu nusu milioni kupoteza makazi yao na kuiharibu miundo mbinu. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, amesema.

´Nimewatolea mwito wote wanahusika kuyalinda maisha ya raia na miundombinu kwa sabu itahijika na umma katika siku za usoni kw amaisha yao ya kila siku. Na hatupaswi kuendelea kuwatesa raia.´

Wajerumani takriban 300 wamerudishwa nyumbani na serikali ya mjini Berlin imesema itawarudisha raia wengine kutoka Lebanon katika siku chache zijazo.