1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT Mwanasiasa wa Lebanon auwawa katika shambulio la bomu

22 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF1D

Mwanasiasa wa Lebanon anayeipinga Syria ameuwawa kufuatia shambulio la bomu katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut. George Hawi, kiongozi wa zamani wa chama cha kikomunisti cha Lebanon, alifariki dunia katika mripuko huo na dereva wake pamoja na wapita njia kadhaa wakajeruhiwa vibaya.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Bi Condoleezza Rice, ametangaza kwamba Syria imechangia kwa njia moja au nyengine katika mauaji hayo ya hivi punde nchini Lebanon. Lakini rais wa Lebanon, Emile Lahoud, anayeiunga mkono Syria, ameyakanusha madai hayo akisema hayana nia nzuri juu ya serikali yake.

Shambulio hilo limetokea siku mbili tu baada ya muungano mkubwa wa upinzani nchini Lebanon kushinda kwa wingi wa viti vinane bungeni.