1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Msaada wa Marekani waimarisha majeshi ya Lebanon

26 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxz

Marekani imepeleka misaada zaidi kwa majeshi ya Lebanon,huku vikosi vya serikali vikiendelea kupambana na kundi la wanamgambo,ndani ya kambi ya wakimbizi wa Kipalestina, ya Nahr al-Bared kaskazini mwa nchi.Ndege tatu za shehena za jeshi la Marekani,zimetua kwenye uwanja wa ndege wa Beirut na kushusha silaha na zana zingine kwa ajili ya majeshi ya serikali.Maelfu ya watu wamekimbilia kambi za jirani na kwengineko kujiepusha na mapigano.Hii leo,kama wakimbizi 150,wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto, waliondoka kambi ya Nahr al-Bared.Shirika la kimataifa,UNICEF limetoa mwito kuwalinda kama raia 10,000 walionasa kambi ya Nahr al-Bared na kutoa nafasi ya kupeleka misaada ya kiutu.