BEIRUT: Mikati atajwa kama waziri mkuu mteule wa Lebanon
16 Aprili 2005Matangazo
Rais Emile Lahoud wa Lebanon amemtaja Najib Mikati kama waziri mkuu mteule wa nchi hiyo.Hati iliyotolewa na ofisi ya Lahoud imesema rais amemualika waziri huyo wa zamani anaeiunga mkono Syria kuunda serikali mpya.Tangazo hilo limetolewa siku moja baada ya rais Lahoud kuwa na majadiliano pamoja na wabunge.Mikati anaesemekana kuwa na siasa za wastani,anatazamiwa kuiongoza nchi mpaka utakapofanywa uchaguzi wa bunge mwezi ujao.Lebanon haina serikali tangu mwezi wa Februari,baada ya waziri mkuu Omar Karami kujiuzulu kufuatia mauaji ya waziri mkuu wa zamani Rafik al-Hariri.