Beirut. Mchunguzi wa kifo cha Hariri arejea Lebanon.
2 Novemba 2005Matangazo
Mjumbe wa umoja wa mataifa anayechunguza kuuwawa kwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri amerejea nchini humo akiwa na mamlaka mapya.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limepitisha azimio ambalo linatoa mamlaka mapya kwa Detlev Mehlis.
Azimio hilo linaitaka Syria kumkamata mtu yeyote ambaye wachunguzi wa umoja wa mataifa wanamuona kuwa ni mtuhumiwa.
Mehlis , ambaye mamlaka yake yamerefushwa hadi Desemba 25, anawezekana akajaribu kumhoji kaka na shemejie rais wa Syria Bashar al – Assad.
Watu hao wawili wametajwa kuwa huenda wanahusika katika kifo cha Hariri.