1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT. Manowari za kivita za Israel zatanda katika pwani ya Lebanon

13 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG7x

Israel imepeleka manowari zake za kijeshi katika pwani ya Lebanon na kuzi zingira bandari zote za nchi hiyo.

Msemaji wa Israel amesema hatua ya kuweka vizuizi katika bandari za Lebanon inanuia kudhibiti usafirishaji wa silaha za makundi ya kigaidi nchini Lebanon.

Hatua hii imefuatia muda mchache baada ya majeshi ya Israel kuushambulia uwanja wa kimataifa wa ndege katika mji wa Beirut na kuulazimu uwanja huo kufungwa.

Takriban watu 40 wameuwawa katika shambulio ya angani huko kusini mwa Lebanon.

Wakati huo huo wanamgambo wa Hizbollah wamesema kwamba wamehusika na mashambulio ya roketi katika mji wa Kiryat Shmona kaskazini mwa Israel.

Mapigano yalizuka kusini mwa Lebanon jana baada ya wanamgambo wa Hizbollah kushambulia maeneo ya mpakani wanajeshi wanane wa Israel waliuwawa na wawili wakatekwa.