BEIRUT; makomando wa Israel wapambana ana kwa ana na Hezbollah kusini mwa Lebanon
5 Agosti 2006Matangazo
Makomando wa Israel leo wamepambana na wapiganaji wa Hezbollah katika msako waliofanya kwenye mji wa Tyre kusini mwa Lebanon ambako wanamgambo wa Hezbollah wanarushia makombora yao ya masafa marefu
Jeshi la Israel limetaarifu kwamba askari wake wanane walijeruhiwa katika mapambano hayo.
Wakati huo huo ndege za Israel zimeendelea na mashambulio nchini Lebanon kote. Msemaji wa jeshi la Israel ameeleza kuwa ndege hizo zilifanya mashambulio zaidi ya 70 katika kipindi cha saa 24 zilizopita.