1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Majeshi yatumia silaha nzito kupambana na wanamgambo Lebanon.

2 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvW

Majeshi ya Lebanon yametumia silaha nzito nzito kushambulia maficho ya wanamgammbo wa Kiislamu kwenye kambi ya wakimbizi wa Kipalestina karibu na mji wa Tripoli.

Kiasi wanajeshi wawili zaidi wa Lebanon wameuawa kwenye mapambano hayo ambayo ni makali zaidi tangu harakati za kijeshi zilipoanzishwa dhidi ya wanamgambo wa Fatah al-Islam wanaosemekana wana mafungamano na mtandao wa al-Qaeda.

Kiiongozi mmoja mkuu wa Fatah al-Islam amesema wapiganaji wake wameondoka kutoka baadhi ya maeneo ya kambi ya wakimbizi ya Nahr al-Barid lakini akarejea msimamo wa kundi lake kwamba halitajisalimisha kwa majeshi ya Lebanon.

Majeshi ya Lebanon yamewataka wakazi wa kambi hiyo kutowapa hifadhi wanamgambo hao.