BEIRUT: Machafuko zaidi Lebanon
5 Juni 2007Matangazo
Takriban watu saba wamejeruhiwa baada ya basi moja lililokuwa limeegeshwa kulipuka mashariki mwa mji mkuu wa Libnan, Beirut.
Hu uni mlipuko wa nne lutokea tangu mapigano yalipoanza kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa kundi Fatah al Islam karibu na mji wa kaskazini wa Tripoli.
Kundi la wapiganaji wa Fatah al Islam linaminika kuwa limo ndani ya kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Nahr al Bared.
Kambi ya pili ya wakimbizi wa Kipalestina ya Ain al Helweh iliyo kusini mwa Libnan katika mji wa Sidon pia iamekubwa na machafuko.
Wapiganaji wa wa kundi la Jund al Sham wana aminika kuhusika na ghasia hizo.