1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Machafuko yazuka tena kaskazini mwa Lebanon

3 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSx

Milio ya risasi na milipuko imesikika karibu na kambi ya wakimbizi ya Nahr el Bared kaskazini mwa Lebanon hii leo.

Machafuko hayo mapya yamezuka huku wanajeshi wa Lebanon wakiendelea kuwasaka wanamgambo wa kundi la Fatah al Islam waliosalia katika pwani ya kaskazini mwa nchi hiyo.

Harakati hiyo inafanyika baada ya jeshi la Lebanon kufaulu kuwafukuza wananamgambo wa kundi hilo kutoka kambi ya wakimbizi ya Nahr el Bared baada ya kuizingira kwa siku 100. Watu takriban 250 waliuwawa wakati wanajeshi walipokuwa wakikabiliana na wanamgambo waliokuwa ndani ya kambi hiyo.

Maafisa wa jeshi la Lebanon wanasema wanamgambo 37 na wanajeshi watatu waliuwawa wakati wanamgambo wa Fatah al Islam walipojaribu kukimbia kutoka kambi ya Nahr el Bared jana alfajiri.

Imeripotiwa kwamba wanamgambo 20 wamekamatwa. Waziri mkuu wa Lebanon, Fuad Siniora, amesema kumalizika kuzingirwa kambi ya wakimbizi ya Nahr el Bared ni ushindi mkubwa dhidi ya ugaidi.