1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT. Maandamo ya kutaka umoja wa taifa yafanywa Lebanon.

11 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFOL

Watu wasiopungua elfu 20 wamefanya maandamano nchini Lebanon wakitaka umoja wa taifa lao. Raia kutoka kila pembe za nchi hiyo walishiriki katika maandamano hayo yaliyoanzia katika kaburi la marehemu waziri mkuu wa zamani, Rafik Hariri, aliyeuwawa miezi miwili iliyopita. Kifo chake kilizusha mzozo wa kisiasa uliosababisha serikali ya Lebanon, inayoegemea upande wa Syria, kukabiliwa na shinikizo, nayo Syria ikalazimika kuamua kuwaondoa wanajeshi wake wote kutoka Lebanon kufikia mwisho wa mwezi huu. Habari zaidi zinasema kiongozi wa upinzani Walid Jumblatt amekataa kucheleweshwa kwa uchaguzi na akayatolea wito makundi ya upinzani kuandaa programu ya kisiasa ya Lebanon baada ya uchaguzi mkuu kufanyika mwezi Mei. Waziri mkuu wa Syria, Omar Karami, anatarajiwa kutangaza serikali mpya hii leo kuliongoza taifa hilo kuelekea uchaguzi. Lakini kusisitiza kwake kutaka sheria mpya ya uchaguzi huenda kukauchelewesha uchaguzi huo.