Beirut. Maandamano yamtaka rais wa Lebanon ajiuzulu kufuatia kifo cha mwandishi wa habari mashuhuri nchini humo.
4 Juni 2005Watu wanaounga mkono upinzani wameingia mitaani katika mji mkuu wa Lebanon Beirut, wakidai kujiuzulu kwa rais anayeiunga mkono Syria Emile Lahoud. Hii inakuja siku moja baada ya mwandishi habari maarufu anayeipinga Syria Samir Qassir kuuwawa katika shambulio la bomu.
Mamia ya waandishi wa habari walifanya maandamano wakiwa kimya, wakishika kalamu nyeusi wakiashiria uhuru wa vyombo vya habari.
Serikali ya Marekani imekitaka kikundi cha umoja wa mataifa kinachochunguza kuuwawa kwa waziri mkuu wa zamani Bwana Rafik Hariri mwezi wa Februari kupanua uwigo wa uchunguzi wao na kujumuisha kifo cha Bwana Qassir. Syria inalaumiwa kwa kifo cha Bwana Hariri. Mbinyo kutoka jumuiya ya kimataifa na upande wa upinzani ambao ulifuatia kifo hicho , ulisababisha Syria kuondoa majeshi yake nchini Lebanon kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka karibu 30.