BEIRUT. Lebanon yazidi kushambuliwa
7 Agosti 2006Israel imeongezea kampeni yake ya kupigana na wanamgambo wa Hizbollah huko kusini mwa Lebanon.
Makomando wa jeshi la Israel wameshambulia sehemu zinazoaminika kuwa za wapiganaji wa Hizbollah kusini mwa mji Tyre huku ndege za kivita za Israel zikishambulia maeneo ya kusini mwa Beirut taakriban watu 20 wameuwawa katika mashambulio hayo mapya.
Mapema leo mwanajeshi mmoja wa Israel aliuwawa na wengine wanajeshi watatu wamejeruhiwa kkatika mji wa Bint Jbeil kusini mwa Lebanon.
Wasambaza misaada wamesema kwamba imekuwa vigumu kusambaza misaada ya kibinadamu baada ya kivukio kilichobaki katika mto wa Litani kuelekea katika mji wa Tyre kushambuliwa na kuharibiwa.
Serikali ya Lebanon imesema kwamba watu 925 wameuwawa kufuatia mashambulio yanayo tekelezwa na majeshi ya Israel na takriban watu 75 hawajulikani walipo.