BEIRUT. Lebanon yasimamisha amri ya kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani wa kikristo.
5 Mei 2005Matangazo
Lebanon imeisimamisha waranti ya kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani wa kikristo aliye uhamishoni nchini Ufaransa, Michel Aoun, na pia kuchelewesha kutolewa kwa hukumu ya kesi ya mwaka wa 2003 inayomkabili. Hatua hiyo imemfungulia mlango kiongozi huyo kuweza kurejea nyumbani kutoka Ufaransa.
Aoun anakabiliwa na mashtaka kuhusiana na ushahidi alioutoa mbele ya kamati ya bunge la Marekani mwezi Septemba mwaka wa 2003, ambao inasemekana uliuharibu uhusiano kati ya Lebanon na Syria.