1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Lebanon yaomba msaada wa Umoja wa amataifa kuyachunguza mauaji ya waziri wake wa viwanda, Pierre Gemayel

23 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqJ

Waziri mkuu wa Lebanon, Fuoad Siniora ameuomba Umoja wa mataifa kusaidia katika uchunguzi juu ya mauaji ya waziri wa viwanda, Pierre Gemayel.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Kofi Annan, amelitumia barua baraza la usalama la Umoja wa mataifa, la kuliomba lijibu ombi hilo la serikali ya Lebanon kwa kuchukuwa hatua inayofaa.

Gemayel aliuawa wakati akisafiri ndani ya gari lake mjini Beirut hapo juzi. Mauaji hayo yametokea wakati tume ya Umoja wa mataifa imekuwa ikichunguza juu ya mauaji ya aliekuwa waziri mkuu wa Lebanon, Rafic Hariri mwaka jana, na baraza la usalama la Umoja wa mataifa lilipitisha pendekezo la kuundwa mahakama itakaowahukumu washukiwa wa mauaji hayo. Wakati huo huo, ma mia ya waombolezaji wamekwenda nyumbani kijijini kwake Gemayel, mashariki ya Beirut kutoa heshima za mwisho kwa mwanasiasa huyo mkristu na mpinzani wa Syria.