1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Lebanon yakumbuka mauaji ya Hariri

14 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSJ

Usalama umeimarishwa mjini Beirut huku umati mkubwa wa watu ukikumbuka miaka miwili ya mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri, aliyeuwawa kwenye shambulio la bomu.

Waandamanaji wanaoipinga Syria, na ambao wanaituhumu serikali ya mjini Damascus kwa kuhusika na mauaji ya Hariri, wanapanga kukusanyika kwenye kaburi lake katikati mwa Beirut.

Wakati huo huo, upinzani, wakiwemo wafuasi wa kundi la Hezbollah, wanapanga nao kufanya maandamano yenye lengo la kuiangusha serikali ya waziri mkuu Fouad Siniora.

Kumbukumbu ya leo inafanyika siku moja baada ya watu watatu kuuwawa na wengine 30 kujeruhiwa wakati mabasi mawili ya abiria yaliposhambuliwa kwa mabomu kaskazini mashariki mwa mji mkuu Beirut.