BEIRUT: Lebanon yajitayarisha kwa uchaguzi mkuu
28 Mei 2005Matangazo
Wapiga kura nchini Lebanon,wanajitayarisha kwa uchaguzi mkuu utakaofanywa siku ya jumapili nchini humo.Chaguuzi zitafanywa katika awamu nne -wa kwanza ukiwa mjini Beirut.Huu ni uchaguzi wa mwanzo kufanywa Lebanon,tangu mwezi uliopita Syria kuondosha vikosi vyake baada ya kuwepo nchini humo kwa miaka 29.Upande wa upinzani unaoipinga Syria unatazamiwa kushinda uchaguzi.Syria iliondoka Lebanon kufuatia maandamano makubwa ya upinzani yaliofanywa nchini humo na pia kushinikizwa na jumuiya ya kimataifa, baada ya kuuawa kwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafiq Hariri.Serikali ya Damascus imelaumiwa na wengi kuwa ilihusika na mauaji hayo.